Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS DK.MWINYI AWAPONGEZA TAASISI YA BENJAMIN W MKAPA KWA UWEKEZAJI WA JENGO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi   amewapongeza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) na kampuni tanzu Imara Horizon kwa fikra sahihi za uwekezaji wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza .

Rais Dk. Mwinyi ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi hiyo amesema  kwa hatua ya uwekezaji wa jengo hilo ambalo litakuwa linatoa huduma za afya  na ofisi  kwa mashirika ya afya ni kielelezo kimojawapo cha mafanikio na kutimiza maono ya kumuenzi Hayati Benjamin William Mkapa.

Ameyasema hayo  leo katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza lililopo Kawe Jijini, Dar es Salaam. 

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendeleza jitihada za kuongeza uwekezaji katika sekta ya Afya hususan katika ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa tiba na upatikanaji wa watumishi wa sekta ya Afya.



Post a Comment

0 Comments