Ticker

7/recent/ticker-posts

DIAMOND AMZIDI ALLY KIBA MGAWO WA COSOTA, WASANII WAKE WAINGIA TANO BORA

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) na wanamuziki wake watatu wamezoa fedha nyingi za mrabaha kutoka  Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (Cosota).

COSOTA hivi karibuni imegawa mirabaha kwa wasanii nchini.

Waliopata fedha nyingi zaidi ni Diamond Platnumz mwenyewe ambaye amepata - Sh. 7.7 milioni, Alikiba - Sh 5.0 milioni, Rayvanny - Sh 4.9 milioni, Zuchu - 4.7 milioni na Mbosso - Sh4.2 milioni.

Kati ya wasanii hao watano ni Ali Kiba pekee ndio hajawahi kuwa sehemu ya Lebo ya WCB huku Mboso na Zuchu bado  wakiwa ndani  ya Lebo hiyo na Rayvan akinitegemea.

Post a Comment

0 Comments