Ticker

7/recent/ticker-posts

MR BLUE AWASHANGAA WANAWAKE WANAOMTONGOZA

"Wanawake bwana, nilijua nikioa watapunguza kunitongoza, lakini sasa baada ya kuoa naona matongozo yamezidi kuwa mengi na nafikiri wamevutiwa na mimi jinsi ninavyokaa karibu na familia yangu kwahiyo wanadanganyika labda nikiwaoa nitawatunza kama ninavyomtunza mke wangu" amesema Mr.Blue

"Lakini hawana nafasi tena kwangu kwasababu niliamua kutulia kidhati, mke wangu amepambana sana kunituliza, mimi kabla ya kumuoa mke wangu nilikuwa na wanawake watatu ambao wote wanajuana, lakini unapoamua kutulia ata mwili wenyewe unakubali kwamba umeamua kutulia, kwahiyo kuna namna lazima ujitoe muhanga"

"Kiukweli mimi namshukuru Mwenyezi Mungu, kwasababu hamna uchafu ambao sikuufanya mke wangu anaujua, yani kiasi kwamba alishawahi hadi kunifumania lakini alinivumilia, kwahiyo imefika kipindi na mimi nataka nimuonyeshe upendo wangu nimeamua kutulia" - Mr. Blue

Mr.Blue amemuoa Waheeda Sylvester pichani ambaye wamezaa watoto watatu, lakini ikumbukwe Najma Dattan aliyewahi pia kuwa mpenzi wa Mr.Blue kabla hajaoa, katika interview aliwahi kusema changamoto kubwa katika mahusiano yake na Mr.Blue ilikuwa ni Mr.Blue kutongozwa sana na kinadada hali ambayo ilikuwa inamnyima furaha Najma enzi hizo na baadaye wakamwagana mazima

Post a Comment

0 Comments