Ticker

7/recent/ticker-posts

MAZITO YAIBUKA SAKATA LA FEISAL, MWENYE WE AKIRI KUIPENDA YANGA

“Tangu zamani nafsi yangu ilinituma niende kucheza Yanga. Nilikuwa natamani kucheza timu kubwa na zilikuja Simba na Yanga pamoja nikachagua kusaini Yanga walionipa kiasi kidogo kuliko ambacho Simba walitaka kunipa. Nilichagua Yanga kutokana na nafsi kunisukuma"

"Kama ningetaka kuvunja mkataba ningevunja ule wa mwanzo kwasababu nilikuwa nakaa miezi mitatu, minne hadi mitano silipwi Mshahara, mama yangu alikuwa ananiambia vumilia mwanangu kwasababu ya hali ya uchumi ya klabu. Mama ni shabiki mkubwa sana wa Yanga"

“Mimi nimetokea kwenye familia ya kimasikini, mimi nasaidia familia yangu, ili mambo yaende ni lazima mimi nifanye kazi, Baba yangu anaumwa na mimi ndio nasimamia matibabu, yeye mwenyewe hapendi hili sakata liendelee kwasababu kuna mambo yanakwama”

"Suala la kulipwa milioni 100 kwa mara moja ni uongo, niliposaini mkataba walinipa Milioni 10, baadae wakanipa Milioni 20. Imekuja kutimia Milioni 100 kwa shida mpaka kugombana,Imechukua miaka miwili kuipata yote"

“Nawapenda mashabiki wa Yanga na nawapa pole maana hawajui kilichoko nyuma yangu. Hawajui kilichonitoa katika timu. Nimeondoka Yanga kwa sababu ya manyanyaso. Niliambiwa nimeuza mechi na nikaambiwa kama sitaki kucheza mpira nirudi kwetu Pemba, nilivumilia. Hata mama yangu alikuwa anadhalilishwa. Mama yangu alikuwa akinipa sana moyo, lakini pia mama yangu ni shabiki mkubwa wa Yanga"

Post a Comment

0 Comments