Ticker

7/recent/ticker-posts

WAZIRI MCHENGERWA ATAKA MISITU NA ASALI KUWA ZAO JIPYA LA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amewataka watendaji wa sekta  ya Misitu na Nyuki  kukamilisha  mkakati wa kuongeza uzalishaji wa asali  toka  tani 35,000 za sasa  hadi tani 138,000  katika kipindi cha miezi miwili alioupa jina la mkakati wa “achia shoka kamata mzinga” huku akitaka eneo la misitu na asali  kufanyiwa utafiti wa kutosha  ili litumike kama zao jipya la utalii.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 21, 2023 wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika kitaifa katika uwanja wa Bombadia mkoani Singida. 

Akiwa kiwanjani hapo amezindua Mwongozo wa Usimamizi wa Hifadhi za nyuki na vibanda maalum vya kuuzia asali pia ametoa Tuzo tano za wadau wenye mchango mkubwa kwenye Sekta ya nyuki na ametoa vyeti kwa wanafunzi walioandika insha nzuri kuhusu ufugaji wa nyuki.

Akisoma hotuba yake, amesema pamoja na uwepo wa maeneo makubwa yaliyohifadhiwa na yanayofaa kwa ajili ya kuzalisha mazao ya nyuki yenye viwango bora bado takwimu zinaonesha uzalishaji ni 23% ikilinganishwa na uwezo uliopo wa kuzalisha tani 138,000 kwa mwaka.

 Kutokana na hali hiyo, waziri Mchengerwa ameielekeza Wizara yake ishirikiane na Wizara ya Kilimo kuanzisha programu za matumizi ya makundi ya nyuki kwenye uchavushaji mimea ili tuweze kuongeza kiwango na ubora wa mazao yanayozalishwa.

Aidha ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mfuko wa Misitu kuhakikisha wanawezesha wananchi hasa wale wanaopakana na maeneo ya hifadhi kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji nyuki pamoja na mizinga ya kisasa. Pia kushirikiana na wadau mbalimbali kuhamasisha jamii kupanda na kuitunza miti katika maeneo yao.

Post a Comment

0 Comments