Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeondoa ukomo wa matumizi wa vitambulisho vya taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NIDA imeeleza kuwa sasa wananchi wote wenye vitambulisho vya taifa ambavyo vina tarehe ya ukomo wa matumizi waendelee kutumia hata kama tarehe inaomesha kimemaliza muda wake.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, baada ya kufanyia marekebisho kanuni ya 7(2) (v) ya kanuni ya usajili na utambuzi wa watu za mwaka 2014.
Uamuzi huo unakwenda sambamba na ombi kwa watoa huduma wanaotumia vitambulisho vya taifa katika kuwahudumia wananchi kuendelea kutoa huduma bila kujali ukomo wa tarehe ya kitambulisho.
0 Comments