Rais Macron akiwa na Rais Xi |
RAIS wa Ufaransa, Ammanuel Macron ameonesha dhamira ya kuishawishi Jumuiya ya Ulaya kuachana na Marekani hasa kwenye migogoro yake na mataifa mengine.
Macron amesema ni lazima Ulaya sasa ipinge shinikizo la kuwa ‘wafuasi wa Marekani,’ na kwamba hatari kubwa inayowakabili ni kunaswa katika majanga ambayo hayawahusu.Ameyasema hayo katika mahojiano aliyoyafanya kwenye ndege yake akirejea kutoka China.
“Ulaya inapaswa kupunguza utegemezi wake kwa Marekani na kuepuka kuingizwa katika mzozo kati ya China na Marekani kuhusu Taiwan.”
Akizungumza na POLITICO na waandishi wa habari wawili wa Ufaransa baada ya kukaa karibu saa sita na Rais wa China Xi Jinping wakati wa safari yake, Macron alisisitiza nadharia yake kipenzi ya "uhuru wa kimkakati" kwa Ulaya.
Alisema hatari kubwa inayokabili Ulaya ni kkunaswa katika migogoro ambayo si yao, ambayo inaizuia kujenga uhuru wake wa kimkakati.
Aliyasema hayo akiwa safarini kutoka Beijing hadi Guangzhou, kusini mwa China, kwa ndege ya Rais ambayo inajulikana kama COTAM Unité, Ufaransa Air firce one.
Xi Jinping na Chama cha Kikomunisti cha China wameidhinisha kwa shauku dhana ya Macron ya uhuru wa kimkakati na maafisa wa China mara kwa mara wanairejea katika shughuli zao na nchi za Ulaya.
Viongozi wa vyama na wachambuzi wa mambo mjini Beijing wanasadiki kwamba nchi za Magharibi zimedorora kiuchumi na China inazidi kuimarika na kwamba kudhoofisha uhusiano wa kupita Atlantiki kutasaidia kuharakisha mwelekeo huu.
Hata hivyo Macron alionesha hofu kwa kusema kuwa viongozi wengi wa nchi za Ulaya wanaamini wao ni wafuasi wa Marekani.
"Hebu tujiulize, tuna sababu ya kuchochea mgogoro wa Taiwan, mimi nasema hapana, jambo baya zaidi lingekuwa kufikiri kwamba sisi ni lazima tuwe wafuasi wa mada hii ya uhuru wa kimkakati na kuchukua tahadhari yetu kutoka kwa ajenda ya Marekani na kuungana na Wachina, "alisema.
Saa chache baada ya ndege yake kuondoka Guangzhou kurejea Paris, China ilizindua mazoezi makubwa ya kijeshi kuzunguka kisiwa kinachojitawala cha Taiwan, ambacho China inadai kuwa ni eneo lake, lakini Marekani imeahidi kukipa silaha na kukilinda.
Mazoezi hayo yalikuwa ni jibu la ziara ya kidiplomasia ya siku 10 ya Rais wa Taiwan Tsai Ing-Wen katika nchi za Amerika ya Kati iliyojumuisha mkutano na Spika wa Bunge la Republican la Marekani Kevin McCarthy alipokuwa akipitia California.
Watu wanaofahamu mawazo ya Macron walisema alikuwa na furaha kwamba Beijing ilingoja angalau atoke nje ya anga la China kabla ya kuzindua zoezi la mfano la "kuzingira Taiwan".
Beijing imetishia kuivamia Taiwan mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni na ina sera ya kukitenga kisiwa hicho cha kidemokrasia kwa kulazimisha nchi zingine kukitambua kama moja ya sehemu ya China.
MAZUNGUMZO JUU YA TAIWAN
Macron na Xi waliijadili Taiwan kwa kina kulingana na maafisa wa Ufaransa wanaoandamana na rais, ambaye anaonekana kuchukua njia ya maridhiano zaidi kuliko Marekani au hata Umoja wa Ulaya.
"Utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan ni wa umuhimu mkubwa," Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen, ambaye aliandamana na Macron kwa sehemu ya ziara yake, alisema alimwambia Xi wakati wa mkutano wao huko Beijing Alhamisi iliyopita kuwa tishio la matumizi ya nguvu litakalobadili hali iliyopo halikubaliki.
Xi alijibu kwa kusema mtu yeyote ambaye alifikiri kuwa anaweza kushawishi Beijing juu ya Taiwan alidanganywa. Macron anaonekana kukubaliana na tathmini hiyo.
“Kama Ulaya hawawezi kutatua mgogoro wa Ukraine sasa tunawezaje kusema kwa uhakika juu ya Taiwan, tunawezaje kumwambia ajihadhari na akifanya jambo baya tutakuwa nae? Ikiwa tunataka kuongeza mivutano hiyo ndiyo njia ya kufanya, lakini mimi sioni kama kuna haja ya kufanya hivyo, "alisema.
"Ulaya iko tayari zaidi kukubali ulimwengu ambao China inakuwa nchi kuu ya kikanda," alisema Yanmei Xie, mchambuzi wa jiografia katika Gavekal Dragonomics.
"Baadhi ya viongozi wake hata wanaamini kwamba utaratibu kama huo wa ulimwengu unaweza kuwa na faida zaidi kwa Ulaya."
Katika mkutano wake wa pande tatu na Macron na von der Leyen Alhamisi iliyopita huko Beijing, Xi Jinping alijikita katika mada mbili tu - Ukraini na Taiwan - kulingana na mtu aliyekuwepo kwenye chumba hicho.
"Xi amekasirishwa na namna mzozo wa Ukraine unavyochochewa na hatua hiyo ilimfanya kuachana na ziara yake Moscow."
"Ni wazi alikasirishwa na Marekani na alikasirishwa sana na Taiwan, hasa kitendo cha ndege ya rais wa Taiwan kupitia Marekani na ukweli ni kwamba masuala ya sera za kigeni ni kama yanamilikiwa na Ulaya, wao ndio wanataka waziamulie nchi zote."
Katika mkutano huu, Macron na von der Leyen waliungana na China juu ya Taiwan, lakini Macron baadaye alitumia musa wa zaidi ya saa nne kuzungumza na Rais wa China na kauli zao zilikuwa za upatanisho zaidi.
Rais Macron
ONYO KWA ULAYA
Macron alioa onyo kwa Ulaya na kusema kuwa imeongeza utegemezi wake kwa Marekani kwa silaha na nishati na lazima sasa kuzingatia kuimarisha viwanda vya ulinzi vya Ulaya.
Pia alipendekeza Ulaya kupunguza utegemezi wake juu ya dola ya Marekani lengo ku likiwa ni kukubaliana na sera ya Moscow na Beijing.
Macron kwa muda mrefu amekuwa mtetezi wa uhuru wa kimkakati wa Ulaya.
"Ikiwa mivutano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu zaidi itaongezeka ... hatutakuwa na wakati wala rasilimali za kufadhili.
Uhuru wetu wa kimkakati ni muhimu, sisi tukiingia tutakuwa ni kama vibaraka," alisema.
Urusi, China, Iran na nchi nyingine zimekumbwa na vikwazo vya Marekani katika miaka ya hivi karibuni ambavyo vinatokana na kukataa mfumo wa kifedha wa kimataifa unaoongozwa na dola.
Baadhi ya viongozi wa nchi za Ulaya wamelalamika kuhusu ‘silaha’ ya dola inayotumiwa na Washington, ambayo inalazimisha makampuni ya Ulaya kuacha biashara na kukataa uhusiano na nchi mahasimu wa Marekani na kama wakilazimisha basi wanakabiliwa na vikwazo vinavyolemaza.
Akiwa amekaa kwenye chumba cha ndege yake cha A330, Macron alidai kuwa tayari "ameshinda vita vya kiitikadi juu ya uhuru wa kimkakati" kwa Ulaya.
Hakuzungumzia suala la uhakikisho wa usalama unatolewa na Marekani kwa Bara hilo, ambalo linategemea sana usaidizi wa ulinzi wa Marekani huku kukiwa na vita kuu vya kwanza vya ardhi barani Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Kama mmoja wa wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi pekee yenye nguvu za nyuklia katika Umoja wa Ulaya, Ufaransa iko katika nafasi ya kipekee kijeshi.
Nchi hiyo imechangia kidogo sana katika ulinzi wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi kuliko nchi nyingine nyingi.
Kama ilivyo kawaida nchini Ufaransa na nchi nyingine nyingi za Ulaya, ofisi ya Rais wa Ufaransa, inayojulikana kama Ikulu ya Elysée, ilisisitiza kuangalia na "kusahihisha" nukuu zote za rais zitakazochapishwa katika nakala hii kama sharti la kukubali mahojiano. Hili linakiuka viwango na sera za uhariri za POLITICO, lakini tulikubaliana na masharti hayo ili kuzungumza moja kwa moja na rais wa Ufaransa. POLITICO ilisisitiza kuwa haiwezi kuwahadaa wasomaji wake na haitachapisha chochote ambacho rais hakusema.
Nukuu katika nakala hii zote zilisemwa na rais, lakini sehemu zingine za mahojiano ambayo rais alizungumza waziwazi zaidi juu ya Taiwan na uhuru wa kimkakati wa Ulaya zilikatwa na Elysée.
0 Comments