Ticker

7/recent/ticker-posts

SIMBA YAIKERA YANGA NDANI YA RAMADHANI

Timu ya Simba, imeonesha ukubwa wao mbele ya Yanga baada ya kuichapa bao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yameifanya Simba kuongeza kasi ya kuwakimbiza mahasimu wao kileleni.  

Simba waliuanza mchezo kwa kasi ya ajabu na katika dakika ya 2, milinzi hodari Henock Inonga Baka aliwanyanyua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao safi kwa kichwa akimalizia Krosi ya Shomari Kapombe.

Bao hilo liliiamsha zaidi Simba na waliendelea kuishambulia Yanga hadi  dakika ya 32, ambapo kiungo fundi Kibu Denis Prosper alipopigilia msumari wa pili kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Yanga  Diarra.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha pointi 63 huku Yanga ikiendelea kuongoza Ligi kwa kuwa na alama 68.

Miamba hiyo ya soka nchini Kila moja imebakiza mechi nne za Ligi Kuu.

Yanga ili wautetee ubingwa wao wanahitaji kushinda mechi tatu ili wafikishe Pointi 76 ambazo Simba akishinda mechi zake zote atakomea pointi 75 .

Post a Comment

0 Comments