BAADA ya mahkama kubaini kuwa mchezaji wa kimataifa wa PSG na timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi hana chochote anachomiliki, hatimae mchezaji huyo ametaka apate mgawo kutoka kwenye mali za mke wake huyo aliyeomba talaka.
Hakimi ambaye amekuwa gumzo duniani kutokana na hatua yake y kukabidhi mali zake zote kwa mama yake amemgeuzia kibao mkewe na kutaka apate gawio kutoka kwenye kali za aliyekua mkewake Hiba Abouk baada ya kutalikiana.
Hiba Abouk ni Mwanamitindo wa Hispania na ana utajiri wa dola milioni 5 ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania bilioni 12.
Hakimi amedai kuwa baada ya talaka amebaki bila kitu na hajui ataishije, huku yeye akiwa ni sehemu ya utajiri wa Hiba, hivyo anaiomba Mahakama imuelekeze aliyekua mkewake amgawie nusu ya utajiri wake ambao ni $2.5M sawa na TZS 6 Bilioni.
Wawili hao walioana mwaka 2018, na wana watoto wawili.
0 Comments