Ticker

7/recent/ticker-posts

WATALII 715 WAVUTWA NA ROYAL TOUR

Meli kubwa na ya kifahari  ya MV Seabaorn Sojourn imetua jijini Dar es Salaam ikiwa na watalii 715.

Meli hiyo iliyotengenezwa Genoa nchini Italia, imetia nanga jijini Dar es Salaam ikitokea visiwa vya Zanzibar ilikoanzia ziara yake nchini Tanzania mapema mwezi huu.


Watalii hao kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajia kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii.

Maeneo hayo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Ngorongoro, Serengeti na Makumbusho ya Taifa, Kijiji cha Makumbusho, Soko la Vinyago la Mwenge pamoja na soko la uchoraji Sanaa za Tingatinga.





Post a Comment

0 Comments