"Kusaidia watu ni kitu ambacho Mungu ameniongoza kukifanya kwa moyo, na ilikuwa ni ahadi yangu kwa Mungu miaka mingi sana wakati nilipokuwa na kipato cha kawaida sana nilikuwaga nikamwambia Mungu siku moja ukinipa fedha napenda nisaidie kila mtu, yalikuwa ni maono yangu, ilikuwa ni kilio cha moyo wangu hata wakati ule nilipokuwa na suluali mbili na shati mbili nilikuwa nampa moja mtu nabaki na moja"
"Nilikuwa napenda kuona na wengine wanafanikiwa, sikupenda kujiona kama nafanikiwa mimi halafu wengine wanakuwa duni, nilipenda kuwashirikisha wengine baraka ambayo inapita kwenye mkono wangu na ninadhani ni wito ambao sisi wote tunapaswa kuwa nao kwenye maisha, kwakweli nataka niwambie ukweli hili jambo ni la kweli hata wewe utajua ni kweli"
"Kutoa siyo kitu rahisi nataka ujue hilo, na ukiona mtu anatoa hawezi kutoa kujifanya, kama inawezakana naomba embu mjifanye kila mtu atoe milioni moja moja sasa hivi yani ghafla tu, siyo rahisi, kutoa ni moyo kutoa ni wito tena wito kama Mchungaji anavyoitwa kumtumikia Mungu, yani unapoona mtu anatoa anamsaidia mwingine halafu mwingine anasema anajionyesha, jamani!! basi kama ni hivyo watu wengi wangejionyesha dunia hii"
"Watu wasingekuwa na matatizo duniani, hivi kuna mtu hapendi kujulikana? kila mtu anapenda kujulikana watu wangejionyesha, lakini nataka niwahakikishie kutoa siyo rahisi!! Unapotoa unaondoa sehemu ya nguvu yako kwenye maisha yako inaenda kwa mtu mwingine, inaenda kujenga maisha ya mtu mwingine, nikitoa milioni moja nikakupa bure ili wewe uitumie kwa ajili ya maendeleo nakuwa nimeondoa sehemu ya nguvu yangu nikakupa wewe ili ikusaidie kupiga hatua"
"Kutoa siyo kitu rahisi, kutoa ni wito!! Ndiyo maana wengi wanavyo lakini wachache ndio wanatoa, na mtu anapotoa usitake kuuharibu moyo wake ukikuta mtu ni mtoaji usijaribu kuuharibu moyo wake, nimeona kuna watu wengine wakiikejeli misaada ninayotoa, wengine ni watumishi wa Mungu kabisa, mwingine unampa anarudi tena kuanza kulalamika angeniongeza zaidi yeye anauwezo"
"Kwahiyo hapo nafikiria labda niache kusaidia binadamu nifanye vitu vyangu maana na mimi nina mambo mengi ya kufanya, sasa ukikuta Mchungaji au Askofu akaongea vitu kama hivyo na umemtoa mahali unajisikiaje? lakini kwasababu ni wito, nitafanya, mtu mwenye moyo mwema ni wa kumsaidia ili huo wema uendelee"- maneno ya Nabii Mkuu Geordavie kwa waumini wake.
0 Comments