Ticker

7/recent/ticker-posts

IMAMU ALIYERUKIWA NA PAKA AKIWA ANASWALISHA APEWA TUZO

Imam Walid Mahsas wa msikiti mmoja kule nchini Algeria ambaye wiki iliyopita akiswalisha Swalah ya Taraweeh Paka alimjia na akampanda mabegani aliendelea kuswalisha Swalah licha ya Paka yule kumrukia mabegani na kumbusu kwa Ishara ya upendo apewa heshima kubwa.

Imam huyo Walid ametunukiwa tuzo na serikali ya Algeria chini ya ofisi ya wizara ya masuala ya dini kwa kuonyesha kwake ile picha ya Uislamu ya huruma na upendo kwa wanyama.

Waislamu walitoa maoni tofauti tofauti waliowengi wanasema hii ni miujiza ya Qur'aani Tukufu allaahu Akbar 

Imeshauriwa kuwa  Muislamu hapaswi kutafuta kujulikana na watu bali tafuta kujulikana na Allah Subhanahu wata alaa, Allah akitaka atakutambulisha Watu Bila shaka kwa namna anavyotaka yeye kukutambulisha


Post a Comment

0 Comments