Gari iliyokuwa imebeba mizigo na abiria, inavyoonekana baada ya kupata ajali
AFRINEWS SWAHILI, SONGEA
WAKATI Watanzania na mamilioni ya wakristo duniani wakisherehekea siku kuu ya Pasaka, hali ni tofauti Songea mkoani Rivuma.
Ajali mbaya imetokea usiku wa kuamkiableo na kuchukua maisha ya wafanyabiashara walikuwa wanatoka eneo la Ndongosi wakielekea mnadani Namatui.
Wakiwa katika mwendo uliodaiwa kiwa ni wa kasi gari yao aina ya Fuso ilipoteza mwelekezo nankuvutwa na utelezi na moja kwa moja kutumbukia Mtoni.
Jeshi la polisi mkoani hapa limethibitisha watu 13 kupoteza maisha na wawili ni majeruhi.
Wengi wa waliopoteza maisha imefahamika kuwa ni wengi ni wakazi wa maeneo ya Lizaboni, Ruvuma na Majengo.
Miili imehifadhiwa kwenye hospitali ya Mkoa kwa utambuzi zaidi.
0 Comments