Ticker

7/recent/ticker-posts

WATENGENEZAJI WA MABASI YA YUTONG KUWEKA KIWANDA TZ






Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki

Ubalozi wa Tanzania Nchini China umesema Kampuni ya Kichina inayotengeneza Mabasi ya Yutong inatarajia kufungua Karakana yake jijini Dar es salaam ili kutoa huduma kwa ufanisi kwa Wateja wao.

 

Taarifa hii imetolewa leo Jijini Beijing katika mkutano wa Balozi Mbelwa Kairuki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Yutong Africa ambapo Karakana hii itakuwa na ukubwa wa kuwahudumia Wateja wenye mabasi ya Yutong katika nchi za Afrika Mashariki

 




Uamuzi huu unafungua milango zaidi kwa Tanzania kuendelea kufanya biashara na China ambao inaonekana kumuondoa Msweden katika utawala wa usafiri Tanzania.

 

Soko la  usafirishaji wa abiria kwa sasa limetawaliwa na mabasi yanayotengenezwa nchini China na kampuni za Yutong, Zhongtong, Higer, Sunlong, Golden Dragon na Kinglong.

Post a Comment

0 Comments