Ameandika @swaleh_shrimp.
Tajiri Abramovic anakataa Waini kutoka kwa mhudumu pale VIP na kumwambia " sikuja Munich kwa lengo la kulewa nimekuja kushuhudia mafanikio makubwa ya klabu yangu"
Uwanja ulikuwa umeshainama Sehemu moja, mpira ni Kama vile umeshatolewa pumzi Bayern walishapiga Kona zaidi ya 15, walishalijaribu lango The blues zaidi ya mara 19.
Wakati The Bavarians wanamkimbilia Muller kushangilia goli lake la kichwa dakika ya 83 , Frank Lampard alimuita Young Ryan Betrand na kumwambia "unawaona wale, wamesafiri zaidi ya kilometa 908 waliofika hapa kutoka London hatuwezi kupoteza kwasababu yao." Alimueleza akimuonyesha mashabiki wa Chelsea waliokuwa jukwaani wakimwaga machozi.
Bayern Munich wakiamini shughuli imeisha, Chelsea wanafuta maji tu kibanda umiza Cha Huku nyumbani kusini watu wanainuka na kujikunuta vumbi kwa kusema mchezo umekwisha.
Dakika 88 inapatikana kona ya kwanza kwa Chelsea Juan Mata aliusafirisha mpira hewani na kumkuta Didier hapo ndipo Bwana Alison Bender alisikika akilalamika kwenye kipaza sauti kwa kusema "Ni Didier Drogba labda na mpira wake wa mwisho kupiga kwa Chelsea, Drogba aliyefunga bao la nyumbani dhidi ya Barcelona, Drogba aliyesawazisha hapa Allianz Arena. It's Drogba against Manuel Neur.. Drogbaaa.."
kiniuliza leo kuhusu ubora wa Peter Cech nitakwambia turudi Munich 2012 mikono yake ilifuta penalt ya Robben katika dakika 30 za nyongeza. Naam alikuwa ni Peter Cech aliyeifuta penalt ya Ivica Olic. Alikuwa ni Peter Cech katika milingoti mitatu wakati doto la Schweinsteiger kiungo katili linakula nguzo ya pembeni.
Waandishi wengi pamoja na mashabiki wa timu hasimu tena kutoka Uingereza walizikosoa na kubeza mbinu za Mwalimu Di Matteo za kupaki basi. Alipoulizwa alijibu "Tulipaki basi kwenye barabara tulizojenga sisi Kama wanataka wajenge zao alafu watupangie wapi pa kupaki".
2012 CHELSEA NA UBINGWA WA KWANZA ULAYA NA WA KWANZA KWA JIJI LOTE LA LONDON.
0 Comments