Naam baada ya Zama za mwendazake Mfalme Bob Junior kuzamishwa kupitia mapinduzi ya umwagaji damu yaliyoshuhudia akifurushwa kwenye kiti cha Ufalme kisha kuuawa sasa ni zama mpya za Bob Killer kutawala. Ndio, huu ni mwanzo wa enzi mpya baada ya utawala wa muda mrefu zaidi takriban miaka 8 ya utawala wa Bob Junior.
Bob Killer ni Simba ambaye amepewa jina hilo baada ya kutekeleza mauaji ya kumuua Bob Junior akishirikiana na waasi wenzake 6, tayari anammiliki Mtoto wa mwendazake Bob Junior aitwaye Ritha Marley Kama mke wake.
Taarifa inasema kuwa Bob Killer ambaye ndiye mtawala mpya tangu jana alikuwa na Simba jike Ritha Marley ambaye ni Mtoto wa Marehemu Bob Junior na Leo hii amekubaliwa kuanza kumpanda huku Hali hiyo ikitarajia kudumu kwa kipindi Cha Miezi 2/3 kabla ya Simba Jike kukubali kubeba mimba na kuzaa na mbabe huyo
Kwa Sasa wanafanya tu mapenzi huku jike akiwa anasubilia kuona Kama Dume huyo ndiye atadumu kwenye utawala au atapinduliwa hivyo Ni lazima wakae Miezi 2/3 Kisha akiweza kufikisha kipindi hicho bila kupinduliwa ndipo ataweza kuzaa na kuendeleza kizazi..
Unaendelea kujifunza nini kwenye haya mapinduzi ya umwagaji damu kugombea madaraka?
Itakumbukwa kuwa tangu kifo cha Bob Junior haijaisha hata wiki mbili. Maisha ndivyo yalivyo lazima yaendelee. Usishangae hata wewe hapo binti yako akaolewa na muuaji wako na hata wakafanya ngono maiti yako ingali bado mochwari.
Ndio huenda hata mke wako kipenzi akaolewa hata kabla ya 40 yako kusomwa. Yani hata kabla uume wako uoze kaburini usishangae ukashuhudia ndoa ya mke wako huku duniani wewe ukiwa akhera madukani hapo kwa Shirima au kwa Mborow.
Nini kimekushangaza katika tukio hili?
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
0 Comments