Ticker

7/recent/ticker-posts

KIFO CHA MALU STONCH CHAZUA GUMZO

Marehemu Malu Stonch wakati wa thai wake.

NA MWANDISHI WETU

Mwimbaji nyota wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia, Malu Stonch amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla  jukwaani, hali ambayo imezua gumzo kwani hakuonekana kuwa na hali mbaya ya kiafya.

 

Hali hiyo imetokea katika ukumbi wa Target Mbezi,  Beach, juzi Jumamosi usiku wakati mwimbaji huyo akiwa jukwaani anaimba wimbo wa "Hadija".

Inaelezwa kuwa wakati anaimba wimbo huyo, Malu Stonch alidondoka ghafla na kupoteza fahamu.

 

Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza huku akiwa bado hajitambui, ndipo akakimbizwa Masana Hospital.

 

Mwanahabari na mdau mkubwa wa muziki, MC Petit aliyekuwa miongoni mwa waliomkimbiza Malu Stonch hospital, ameithibitishia Saluti5 kuwa mwimbaji huyo amefariki.

 

"Pale Masana walipompokea tu, wakatumbia tumpeleke Lugalo Hospital kwa kuwa mgonjwa wetu ameshafariki," ameeleza MC Petit.

 

"Tulipofika Lugalo nao wakatuthibitishia kuwa Malu Stonch amefariki na  hivyo tukafanya utaratibu wa kumpeleka chumba cha kuhifadhi maiti," alifafanua zaidi MC Petit. Pumzika kwa amani Malu Stonch.

Post a Comment

0 Comments