Ticker

7/recent/ticker-posts

ALIYEKUWA KAMISHNA WA NCAA ADAIWA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA UMMA

Aliyekuwa Kamishna wa NCAA, Richard Kiiza


NA MWANDISHI WETU

Diwani wa kata ya Alaitole tarafa ya Ngorongoro, James Moringe ameibua tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma kwa aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Richard Kiiza kutumia milioni 400 kwa ajili ya malazi ya hoteli kwa miezi mitatu.

Moringe amedai kuwa Kiiza alitumia shilingi milioni 400 ndani ya miezi mitatu kulala hotelini huku akigoma kuishi katika nyumba aliyokuwa ametengewa kwa ajili yake.

 

Amesema Kiiza ambaye amekwishaondolewa kwenye nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Machi 15,2024 alikuwa akilipa shilingi milioni 3.2 kama gharama ya hoteli kwa siku tangu kuteuliwa kwake Oktoba 2,2023.

 

Baada ya madai hayo Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia walitoa taarifa kwa kudai kuwa wamekwishaanza kufuatilia taarifa hizo hata kabla ya Diwani huyo kuzungumza na Waandishi wa Habari juu ya tuhuma hizo kwa Kiiza.






Post a Comment

0 Comments