Ticker

7/recent/ticker-posts

AJALI ZA MAJINI ZATAWALA AFRIKA

Picha hii ni ya Maktaba haihusiani na ajali yeyote kati ajali mbili zilizozungumziwa kwenye taarifa hiyo haps chini.

NA MWANDISHI WETU

Siku moja baada ya Meli ya Maman Benita  iliyokuwa ikitoka Kigoma nchini Tanzania kuelekea Kalemie nchini DRC kuzama Aprili 7,2024 hatimae leo kivuko kimezama nchini Msumbiji. Ajali ya Meli iliyotokea Tanzania ilidaiwa kuhusisha abiria 25 wakiwemo Wakongo 16, Wachina 4, Watanzania 4, Mkenya 1 na hakukuwa na taarifa ya abiria hao kufariki dunia.

Hata hivyo ajali ya kivuko huko  Msumbiji inadaiwa imehusisha watu takribani 130 na watu watano waliwahi kuokolewa. Imeelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha vifo kwa baadhi ya abiria na miongoni mwao ni watoto na chanzo kikubwa ni uzito kuzidi kwenye kivuko hicho, kilichozama katika eneo la jirani na jimbo la Nampula.

Post a Comment

0 Comments