Ticker

7/recent/ticker-posts

‘KAPTENI’ GADNER G HABASH AFARIKI DUNIA

Marehemu Gadner G. Habash

 
NA MWANDISHI WETU

Ni simanzi kwenye tasnia ya Habari Tanzania baada ya asubuhi ya leo kusambaa kwa taarifa za kifo cha mtangazaji na mwendesha shughuli (MC) mbalimbali Gadner Habash, maarufu kama ‘Kapteni G Habash’.

Habash ambae alijizolea umaarufu kupitia kipindi cha Jahazi cha Clouds Redio akiwa na aliyekuwa swahiba yake, marehemu Ephraim Kibonde amefariki dunia akiwa anaendelea na matababu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya kIKWETE (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.


Imeelezwa kuwa Habash alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda kidogo. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Gadner.

Post a Comment

0 Comments