Ticker

7/recent/ticker-posts

CCM KILOMBERO YAWATAKA VIONGOZI WAKE KUISIMAMIA SERIKALI

 NA VICTOR MAKINDA, KILOMBERO MOROGORO. 

 Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Kilombero, wametakiwa kuisimamia serikali ili iendelee kutekeza ilani ya uchaguzi ya chama hicho. 

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kilombero, Hemed Msuya, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika kwa ngazi ya wilaya Kata ya Msolwa Steheni, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro jana. 

 Msuya amesema kuwa CCM ndiyo chama kilichopata ridhaa ya wananchi ya kuunda serikali kupitia sanduku la kura, hivyo viongozi wa chama hicho wana dhima ya kuwasimamia watendaji wa serikali na kuwawajibisha viongozi wote wanaoendekeza urasimu na ugoi goi katika kuwahudumia wananchi. 

 “ Msiogope, chama ni zaidi ya serikari, kipo juu na serikali ipo chini ya chama. Mjitambue kuwa ninyi ni wasimamizi wa kuwasimamia viongozi wa serikali ili wafanye kazi kwa bidiii kutekeleza ilani ya CCM” Alisema Msuya. 

 Aliongeza kusema kuwa CCM wilayani Kilombero, haitasita kuwachukulia hatua watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi. Akizungumza kuhusu miaka 47 tangu kuzaliwa kwa CCM, Msuya amesema kuwa chama hicho kinajivunia misingi iliyoasisiwa na kuilinda, ikiwa ni uzalendo, utu, umoja na mshikamano wa kitaifa.  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ifakara Mji, wilaya ya Kilombero, Kasim Nakapala, akizungumza kwenye maazimisho hayo, alisema kuwa wakati tunasherehekea miaka 47 ya CCM, Halmashauri ya Kilombero imepokea miradi mingi ya maendeleo hivyo ni wajibu wa watendaji wote wa serikali kusimamia miradi hiyo ili ilete tija kwa wananchi. 

 “ Tunaimshukuru serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea miradi mingi ya maendeleo wilayani kilombero, ikiwa ni miradi ya elimu, afya,kilimo, umeme na ujenzi wa barabara, hivyo watendaji wa serikali wanapaswa kuendana na kasi ya rais katika kusimamia miradi hiyo ili ituletee maendeleo.. Alisema Nakapala.

Post a Comment

0 Comments