Ndumbaro amezungumza na wachezaji hao mara baada ya kushuhudia mazoezi na utayari wa kikosi hicho kuelekea mchezo wao na Timu ya Taifa ya Morocco utakaopigwa jijini humo leo Januari 17, 2024.
Baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa muda wa takribani saa mbili, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema ameridhishwa na maandalizi ya kikosi hicho, Ari na morali ya wachezaji na benchi la ufundi ambayo inatoa picha nzuri ya kufanya vizuri katika kundi F la michuano hiyo.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) ambaye pia ni Mkuu wa msafara wa timu Suleiman Mahamoud Jabir.
0 Comments