Ticker

7/recent/ticker-posts

VIONGOZI WATEMBELEA ENEO LILILOATHIRIWA NA MAFURIKO MANYARA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama leo Novemba 5,2023 wamefika katika kijiji cha Gendambi kata ya Gendambi Wilaya ya Hanang mkoani Manyara eneo yalipotokea mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.

Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni eneo lililoathirika sana na maporomoko ya matope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia Disemba 3,2023.


Post a Comment

0 Comments