Ticker

7/recent/ticker-posts

DCPC YASAMBAZA UPENDO KWA YATIMA

Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) jana Desemba  3,2023 wametembelea kituo cha watoto yatima cha Umra, kilichopo Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam.

Wakiwa kituoni hapo Katibu wa DCPC, Fatma Jalala na  baadhi ya wajumbe walikabidhi vyakula, sabuni, sukari, nguo pamoja na viatu.

Vitu vyote hivyo vimekusanywa kutoka kwa  wanachama wa DCPC kwa  kushirikiana na uongozi wa chama hicho. 

Akizungumza wakati wa kukubidhi  mahitaji hayo Bi.Jalala amesema DCPC itaendelea kurudisha shukurani zake kwa jamii.


"Huu si mwisho wa klabu yetu kurudisha upendo kwa jamii, leo tumeanza na watoto wenye mahitaji, wakati mwengine tutakwenda kurudisha upendo kwa wajane na zoezi hili ni endelevu.”

Adha Bi. Jalala  ameviomba vyama vya kihabari na taasisi mbalimbali nchini kuendelea  kujitokeza  kusaidia jamii zenye uhitaji hata kwa kidogo walichonacho ili kuleta tabasamu kwao.

Amesema kwenye kutoa hakuna kidogo na kwamba DCPC inatarajia kufanya zoezi hilo mara mbili au tatu kwa mwaka.


Kwa upande wake mlezi na mmiliki wa kituo hicho Bi. Rahma Kishumba amesema, kituo hicho kina takribani watoto 700 na waliopo katika kituo hicho ni 400  wakiwemo wa kike na wa kiume kwa rika tofauti.

Post a Comment

0 Comments