Ticker

7/recent/ticker-posts

GAMOND 'ACHUKIZWA' NA UTARATIBU WA KUIPA MECHI JINA LA MCHEZAJI

Kocha Mkuu wa timu ya Yanga Miguel Gamond amesema kuwa hakubaliani na utaratibu wa kuupa jina mchezo kwa sababu mechi inakuwa ni ya wachezaji wote.

"Sikubaliani kabisa na huu utaratibu wa kuita mchezo jina la mchezaji, kwa sababu mchezaji hayupo peke yake wapo timu. Jambo muhimu kwangu ni timu sio mchezaji mmoja, ila naelewa ndio utaratibu wa timu kwa ajili ya kufanya marketing, kuwafanya mashabiki waje uwanjani na kuuelewa zaidi mchezo husika, najua huo ndio utaratibu wa klabu kuhamasisha ila sio utaratibu mzuri kwangu mimi binafsi." amesema Gamondi.

Post a Comment

0 Comments