Ticker

7/recent/ticker-posts

SERIKALI YAITAKA YANGA KUTENGENEZA VITI VILIVYONG'OLEWA UWANJA WA MKAPA

WIZARA ya Utamaduni Sanaa na michezo imewasilisha barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania -TFF ikiitaka Yanga kugharamia matengenezo ya viti na  uharibifu mwengine uliofanywa na mashabiki wao  kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Barua hiyo imeekeza kuwa Wizara ilitoa kibali cha kufanyika kwa mchezo wa kimataifa kati ya Yanga dhidi ya Al-Ahly katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliofanyika Desemba 2 ,2023.

“Hata hivyo, Wizara imepokea malalamiko kutoka kwa uongozi wa uwanja ambapo mashabiki wa klabu ya Yanga wanalalamikiwa kwa kuwasha fataki wakati mchezo ukiendelea na kusababisha vurugu zilizopelekea baadhi ya viti kung’olewa,”

“Wizara inakemea vikali kitendo hiki na kuwataka klabu ya yanga mara moja kuwasiliana na uongozi wa uwanja ili kuweza kubaini ukubwa wa tatizo na kuona namna bora ya kulitatua,”


“Kwa barua hii, Wizara inawasilisha rasmi malalamiko haya kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwa ndiye mdhamini wa vilabu hivi kwa maombi ya matumizi ya uwanja huu ili kuwajulisha Klabu ya Yanga SC kuwa inapaswa kugharamia matengenezo ya viti vilivyong’olewa na mashabiki wakati wa mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments