Ticker

7/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS AWAASA WATANZANIA KUTOITUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Desemba 10,2023 ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili.

Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewaasa watanzania kutumia vema mitandao ya kijamii. Amesema matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.


Post a Comment

0 Comments