Ticker

7/recent/ticker-posts

DCPC YAPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA KWA WAANDISHI WA HABARI

Viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari, mkoa wa Dar es Salaam leo Desemba 10,2023 wamefanikiwa kushiriki Mkutano Mkuu wa Umoja za Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Mkutano huo umefanyika katika ofisi za makao makuu ya  UTPC zilizopo Uzunguni jijini Dodoma.

Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa tathmini uliofanyika Desemba 8,2023 na Desemba 9,2023 kulifanyika maonesha ya klabu zote 28 za wanahabari Tanzania zilizo chini ya mwamvuli wa UTPC.

Katika maonesho hayo DCPC ilijikita kwenye elimu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na wasichana vyuoni na kwenye vyombo vya habari.

Katibu Mkuu wa DCPC, Fatma Jalala, alisema elimu hiyo imeenda sambamba na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambazo kilele chake ni leo.


"Tumetumia vipande vifupi vya filamu tuliyoanza kuiandaa sambamba na makala fupi yenye kuelezea baadhi ya majukumu yetu.

"Huu ni muendelezo wa siku 3 za Mkutano Mkuu wa UTPC ambao leo Desemba 10,2023 ndio siku rasmi ya Mkutano huo. 

"Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano wenu." alisema Jalala.


Post a Comment

0 Comments