Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda na msafara alioambata nao wamejikuta wakimwaga machozi baada ya kumuona Mama aliyejifungua saa chache mara baada ya kuokolewa kwenye tope.
Akizungumza leo alipomtembelea mwanamke huyo katika Kituo cha Afya Gendabi mahali ambapo ndipo kulikuwa na maafa makubwa kufuatia mafuriko yaliyosababisha madhara makubwa Hanang.
"Nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona mwanamama huyu ambaye alisombwa na tope na kuweza kuokolewa kwenye tope hilo na kufikishwa hospital saa mbili baadaye na kujifungua salama.
"Kwa kweli nimelia kwa uchungu baada ya kusikiliza simulizi za mama huyu namna alivyohangaika kuokoa watoto wake wawili na huku akiwa ni mjamzito wa miezi tisa, hakika hakuna kama Mama . Namshukuru sana Mungu kutenda maajabu na kumuwezesha mama huyu kujifungua salama na mtoto yupo Salama na ameitwa Mussa."
Aidha Mwenyekiti wa UWT amesema Jumuiya itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea mahitaji ya kutosha
Mama huyo kwa sasa yeye na familia yake wanalala hospitali kutokana na kukosa makazi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya kutokana na mafuriko ya matope yaliyoikumba baadhi ya maeneo ya wilaya ya Hanang.
0 Comments