Ticker

7/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZIKO YA DC WA ZAMANI WA RUANGWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana  Novemba 12, 2023, amewasili mkoani Lindi kufanya shughuli mbalimbali za kiserikali, ambapo pia ameshiriki kwenye msiba na maziko ya Bi. Fatma Mikidadi.

Bi. Fatma Mikidadi aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa nyakati tofauti. 

Akimzungumzia Bi. Fatma, Waziri Mkuu amesema ni  miongoni mwa viongozi wa awali wa Wilaya ya Ruangwa ambao wameacha alama kwa wananchi wa wilaya hiyo. 

"Enzi za uhai wake  alikuwa miongoni mwa watu waliofanya jitihada kubwa ya kuhakikisha Mkoa wa Lindi unapata maendeleo kwa  kushiriki katika miradi ya kuwainua wananchi."





Post a Comment

0 Comments