Ticker

7/recent/ticker-posts

MAKONDA ATEMBELEA DARAJA LA MAGUFULI

​

Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndg. Paul Makonda ametembelea na kukagua mwendelezo wa Ujenzi wa Daraja la JPM (Kigogo - Busisi) lenye urefu wa Kilomita 3 na Barabara unganishi yenye urefu wa Kilomita 1.66 linalojengwa Wilayani Misungwi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ujenzi  Innocent Bashungwa amemueleza Mwenezi Makonda kuwa Ujenzi wa Daraja hilo umefikia 80% na mpango wa Serikali ni kuhakikisha hadi kufikia mwezi Agosti mwakani 2024 ujenzi utakuwa umekamilika kwa 100%.

Mwenezi Makonda ameitaka Serikali kuhakikisha inaongeza kasi katika utekelezaji wa Mradi huo.




Post a Comment

0 Comments