Ticker

7/recent/ticker-posts

BENCHIKA AANZA KUWATISHA MASTAA SIMBA

Kocha mpya wa Simba Abdelhak Benchika ameanza kuwatisha mastaa wa timu hiyo kwa kusema kuwa kamwe  hatoangalia ukubwa wa majina ya wachezaji wa timu hiyo na kwamba  atakayejituma ndoe atakae atajihakikishia nafasi.

Benchika aliyewasili juzi usiku akitokea Algeria, baada ya kutangazwa kuwa kocha wa timu hiyo siku nne zilizopita amesema kiwango cha mchezaji kitampa nafasi.

Akizungumza na wanahabari leo kocha huyo wa zamani wa USM Alger amesema katika kufanikisha mengi muhimu viongozi, wanachama na mashabiki wafahamu mafanikio yatajengwa na Wanasimba wote.

“Kuna mambo mengi ambayo tayari nayajua na nimekuja na mikakati ambayo tutaifanyia kazi. Kuhusu wachezaji tajua zaidi nikishaanza kazi”

“Kuhusu mashindano ya ndani na kimataifa yote ni muhimu. Mimi ni mpambanaji na nitapambana hadi tutafika”. Benchikha

Post a Comment

0 Comments