Ticker

7/recent/ticker-posts

AJALI YACHUKUA UHAI WA NYOTA WA SOKA WA AFRIKA KUSINI

Nyota wa zamani wa Afrika Kusini Papi Khomane (48), amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari wakati wakielekea msibani.

Ajali hiyo imegharimu pia maisha ya Mama yake Mzazi pamoja na mjomba wake. Watu hao walipoteza maisha wakati wakiendesha kuelekea kwenye msiba huko NewCastle katika jimbo la KwaZulu Natal.

Mlinzi huyo wa zamani wa Bafana Bafana aliwahi kuichezea klabu ya Jomo Cosmos ya Johannesburg. 

Vilevile, yeye pamoja na baba yake Yster waliwahi kuichezea Orlando Pirates FC ya Soweto almaarufu The Buccanners, ambapo Khomane aliwahi kuwa Nahodha wa timu hiyo. 

Alishinda mataji tisa akiwa na Bafana Bafana.Mwaka 2000 aliisaidia timu ya Afrika Kusini kushika nafasi ya tatu katika michuano ya mataifa ya Afrika AFCON.



Post a Comment

0 Comments