Ticker

7/recent/ticker-posts

SIMBA YAZINDUA JEZI ZITAKAZOUMIKA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE

UONGOZI wa klabu ua Simba  umezindua jezi rasmi zitakazotumika kwenye mashindano ya ‘African Football League’ (AFL) inayotarajiwa kuanza  Oktoba 20, 2023.

Mchezo wa ufunguzi utakaozikutanisha  Simba na Al-Ahly ya Misri, utachezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

“Nafurahi kuwambia baada ya uzinduzi wa jezi hii, jezi zitaanza kupatikana kwenye maduka ya Sandaland. Leo wataanza kupendeza,” amesema Salim Abdallah, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba.

Ameishukuru serikali kwa kwa kukubali kufanya marekebisho ya Uwanja wa Mkapa ambao utatumika katika mchezo wa ufunguzi.


Juzi Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alitamba kuwa mashindano ya AFL mwaka huu ambayo yatashirikisha timu 8 Afrika ni maalum kwa ajili ya timu kubwa, huku akisisitiza hiyo ni ligi ya wakubwa.


Post a Comment

0 Comments