Ticker

7/recent/ticker-posts

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI NA KUCHUKUA SANDA

Watu wasiojulikana wamefukua kaburi mwili wa Idd Salum anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22, uliozikwa jana Jumatano Oktoba 11, 2023, katika makaburi ya Waislam mtaa wa Nyahingi kata ya Mkolani jijini Mwanza  na kuondoka na sanda ya marehemu.

Kwa mujibu wa kiongozi katika msikiti wa Khayrudini Mkolani Said Mselem, amesema walifika asubuhi kwa ajili ya swala na kukuta hali hiyo, na kuongeza kuwa huenda waliofanya tukio hilo waliruka ukuta wa fensi ya makaburini hapo,  kisha kufukua kaburi hilo na kuondoka na sanda ya marehemu.

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limefika katika eneo la tukio na baada ya uchunguzi wa awali limeruhusu mwili huo uzikwe tena.

Post a Comment

0 Comments