Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS WA UJERUMANI ATUA NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

 RAIS wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier amewasili nchini usiku wa Oktoba 30, 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akiwa nchini pamoja na mambo mengine Rais Steinmeier atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 31, 2023. 



Post a Comment

0 Comments