Bondia Mtanzania, Pius Mpenda ameshinda ubingwa wa 'WBC Peace Champion' usiku wa kuamkia leo katika pambano lililopigwa Jijini Istanbul Uturuki.
Mpenda ameshinda pambano hilo dhidi ya Dauren Yeleussionov raia wa Kazakhstan kwa pointi za majaji wote.
Ikumbukwe kuwa Januari mwaka huu Mpenda alishinda mkanda wa ubingwa wa Dunia wa WBU dhidi ya Faruku Daku wa Uganda katika pambano lililopigwa nchini Uganda.
0 Comments