Ticker

7/recent/ticker-posts

KINANA AMUAGA ZELOTHE STEVEN KWA MAJONZI NA UJUMBE MZITO

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindizi (CCM), Tanzania Bara,Abdulrahman Kinana amesema maisha ni hadithi, ukitaka kuandika maisha yako uwe na mambo mema kwani  uongozi ni tabia si akili na wala si masomo.

"Kinachomtofautisha mtu katika uongozi ni tabia yake kwani kiongozi ni mtu anayejenga umoja"

Kauli hiyo imetoa katika Ibada ya Kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Arusha, marehemu Zelothe Stephen ambapo amesema

Cheo cha marehemu kilikuwa cha juu sana lakini hakuwa kiongozi wa kutisha watu na watu walimheshimu kwa tabia na alitoa rai kwa viongozi wengine kuweka mkazo katika tabia na si vyeo vyao.

"Mungu atufanye kuwa watu wenye tabia njema na si ukubwa wa vyeo."

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema amepoteza mtu muhimu katika maisha yake na alikuwa ni kiongozi wa aina yake.

Post a Comment

0 Comments