Ticker

7/recent/ticker-posts

MAKONDA ARIPOTI RASMI KWA CHONGOLO, APEWA BARAKA ZOTE

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda leo Oktoba 27,2023 ameripoti rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Daniel Chongolo.

Akimkaribisha Makonda, Katibu Mkuu wa CCM amesema chama  kiko salama na imara katika kusimamia misingi, shabaha na malengo yake, ikiwemo kuendelea kuwa daraja la kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi. 

Amesema kuwa hali hiyo inatokana na jinsi ambavyo CCM kinaendelea kuwatumikia wananchi kwa kuzisimamia Serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambazo zimeendelea kutafsiri maelekezo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kwa vitendo.


Chongolo amesema hayo Alhamis, Oktoba 26, 2023, alipokutana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Ndugu Paul Christian Makonda na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdallah Hamid, walipofika ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya kuonana naye, kujitambulisha na kuanza kazi, baada ya kukabidhiwa ofisi zao rasmi na watangulizi wao. 

Ndugu Chongolo aliwaelekeza Ndugu Makonda na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid, kuanza majukumu yao, wakitambua imani kubwa waliyopewa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndugu  Samia Suluhu Hassan, kutumikia Chama kupitia nafasi hizo walizoteuliwa. 


Ndugu Chongolo amesema kuwa nafasi hizo mbili, Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, ni mojawapo ya maeneo ya kimkakati ya CCM, hivyo wanapaswa kujua kuteuliwa kwao ni sehemu ya kuongeza chachu na kasi ya idara hizo kutekeleza malengo yaliyokusudiwa na CCM, katika kutumikia wananchi na kuzisimamia Serikali zote mbili za CCM. 

“Karibuni  na hongereni  kwa kuaminiwa na kuteuliwa, ujio wenu utakuwa sehemu ya kuongeza kasi ya yale ambayo chama tumekusudia. Uenezi na siasa ndiyo kila kitu,  mmeaminiwa na kuteuliwa kushika maeneo muhimu kafanyeni kazi.


Post a Comment

0 Comments