Ticker

7/recent/ticker-posts

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AANZA ZIARA PEMBA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, jana Jumatano Oktoba 25,  2023 amewasili Kisiwani Pemba, kwa Ziara Maalum ya Siku 4, kwaajili ya Shughuli mbali mbali za chama na Serikali.

Katika Uwanja wa Ndege wa hapa Pemba, Mheshimiwa Othman ambaye ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib,  amepokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa  na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Baada ya kuwasili kisiwani Pemba, Mheshimiwa Othman amefika huko Pandani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini, ili  kumjulia hali Mzee Masoud Juma Haji, pamoja na kufanya Mazungumzo Maalum na Wazee wa Kijijini hapo. 







Post a Comment

0 Comments