Ticker

7/recent/ticker-posts

GAVANA AJITOLEA KIMSOMESHA WAKILI FEKI KENYA

Gavana wa zamani  nchini Kenya, Mike Sonko, amevutiwa na ujasiri wa kijana Brian Mwenda Njagi ambaye amekamatwa kwa tuhuma za kujifanya wakili.

Sonko kupitia ukurasa wake wa X ameeleza kuwa atajitolea kumsomesha Brian kwenye shule ya sheria ikiwa atakosa pesa ya kwendea kusoma.

Leo mamlaka za serikali nchini Kenya zimemkamata Njagi (pichani juu), ambaye amekuwa akijitangaza kwa kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Chama cha Wanasheria cha Kenya (LSK) tawi la Nairobi Rapid Action Team (RAT) kilimkamata tapeli huyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa umma kuhusu shughuli zake za ulaghai.

Kulingana na chama cha wanasheria nchini Kenya, Njagi si wakili na hana ‘leseni’ ya kutekeleza sheria nchini humo.

Brian licha ya kuwa Wakili wa uongo lakini amefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya taarifa zake kujulikana kuwa alishawahi kusimamia kesi 26 na alitoa hoja mbele ya Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Rufani na kushinda kesi zote 26 kabla ya kukamatwa.



Post a Comment

0 Comments