Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi jengo la ghorofa 17 la Makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) lililopo Jijini Arusha ambalo Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 54.
Jengo hilo refu kuliko yote Jijini Arusha linamilikiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Asilimia 40 na Umoja wa Posta Afrika wanamiliki Asilimia 60.
0 Comments