Ticker

7/recent/ticker-posts

CHRISTIAN RONALDO ATOA MSAADA WA KIBINADAMU MOROKO

Mshambuliaji wa soka wa kimtaifa ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Al Nassir ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo ameamua kuitoa hoteli yake ya kifahari ya Pestana CR7 iliyoko Marrakech nchini humo kwa ajili ya kuwahifadhi manusura wa tetemeko lililotokea nchini Morocco na kusabababisha maelfu kufariki dunia.

Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno aliyewahi kuzichezea klabu za Manchester United na Real Madrid amefikia uamuzi huo kufuatia tetemeko la ardhi kutokea nchini Morocco huku likiacha maelfu ya watu kukosa makazi na wengine kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sports Brief, imesema uwezo wa hoteli hiyo ya kifahari ya Pestana CR7 iliyoko M Avenue Marrakech yenye jumla ya vyumba 174 inaelezwa itasaidia manusura wengi katika eneo la mji wa kale wa jiji hilo la kitalii.


Post a Comment

0 Comments