Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameweka wazi kuwa hakuna mtu yeyote atakaekamatwa au kushtakiwa kwa sababu ya kukosoa mkataba wa Bandari.
Nape amesema hayo wakati akitoa ufafanuzi wa kukamatwa kwa Dkt. Willibroad Slaa, Mpaluka Nyangali na Boniface Mwabukusi.
Waziri huyo amesema watu hao wamekamatwa kwa makosa ya uhaini na sio kukosoa mkataba wa uwekezaji bandarini kama inavyoelezwa na wasio jua.
Dkt. Slaa na wenzake hao wanadaiwa kukamatwa kutokana na mazungumzo yao yaliyokuwa na sura ya kuipindua serikali kwa kutaka kuaitisha maandamano.
0 Comments