Ticker

7/recent/ticker-posts

TRA YABORESHA VIWANGO VYA KODI YA MAJENGO

MAMLAKA  ya mapato  Tanzania (TRA)  imeeleza kuwa serikali  imefanya mabadiliko  ya sheria ya serikali  za mitaa ya utozaji kodi ya majengo sura ya  289  kupitia sheria ya fedha ya 2023 ambapo viwango vya  utozaji kodi vimebadilika pamoja na wigo wa ukusanyaji kodi hiyo umeongezeka kwa kujumuisha nyumba zilizopo maeneo ya Wilaya.

Taarifa iliyotolewa na TRA leo Julai 26, 2023 imesema  moja ya mabadiliko hayo ni nyumba ya kawaida iliyokuwa ikitozwa sh 12,000 kwa mwaka sasa itatozwa  sh 18,000 kwa mwaka sawa na sh 1,500 kwa mwezi.

Nyumba za ghorofa katika maeneo ya Majiji, Manispaa  na Halmashauri  za mji zilizokuwa  zinatozwa sh 60,000 kwa kila sakafu kwa mwaka sasa zitatozwa sh 90,000 kwa mwaka sawa na sh 7,500 kwa mwezi.

Taarifa hiyo ya TRA imeongeza  wamiliki wote wanaostahili kupata msamaha wa kodi ya majengo wataendelea kupata msamaha huo kwa kufuata utaratibu ulikuepo awali.

Post a Comment

0 Comments