Ticker

7/recent/ticker-posts

CHUMA CHAVUNJA SHINGO YA BAUNSA NA KUMUUA

Mnyanyua vyuma mwenye umri wa miaka 33 huko Bali Indonesia, Justyn Vicky amefariki baada ya kuvunjika shingo Julai 15 kwenye ukumbi wa mazoezi (GYM).

Justyn alikuwa akifanya mazoezi ya nguvu katika gym ya The Paradise Bali, Sanur, Indonesia, wakati chuma cha uzani wa zaidi ya paundi 450 ambazo ni sawa na kilogram 204, kilipo muangukia shingoni, kulingana na ripoti ya Daily Mail.

Mashuhuda walisema Justyn alipokuwa akijaribu kuchuchumaa na vyuma vizito huku nyuma yake kukiwa na msaidizi wake, wakati chuma hicho kilichomzidia uzito upande wa mbele na kumpelekea aanguke na chuma hicho kuangukia eneo la shingo na kumuumiza vibaya. 

"Uzito ulisogeza kichwa cha Vicky mbele, na kumvunja shingo, na kusababisha mgandamizo wa mishipa kwenye moyo wake na mifumo ya upumuaji," kulingana na Bali Express.

Baada ya ajali hiyo, Justyn alikimbizwa katika hospitali ya eneo hilo akiwa amevunjika shingo.  Alifariki muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura, licha ya juhudi kubwa za madaktari wa upasuaji kuokoa maisha yake.

Post a Comment

0 Comments