Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS DKT. SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JKT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 10,2023 ameshiriki kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri  jijini Dodoma.

Pamoja na ushiriki huo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pia amezindua kitabu cha miaka 60 ya JKT tangu kuanzishwa kwake mwaka Julai 10, 1963. 

Aidja Rais Samia amepokea tuzo maalum kwa mchango wake mkubwa katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) tangu alipoingia madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2021.

Post a Comment

0 Comments