Ticker

7/recent/ticker-posts

PADRI AFIA HOTELINI AKIWA NA MWANAMKE

Padri Joseph Kariuki Wanjiku (43) aliyekuwa Padri wa kanisa katoliki, Parokia ya Mtakatifu Paulo, Jimbo kuu la Nairobi, ameripotiwa kufariki baada ya kupoteza fahamu katika hoteli moja iliyopo  Kaunti ya Murang'a, alipokuwa amepumnzika na mwanamke wa miaka 32 anayetajwa kuwa ni mpenzi wake na pia ni mfanyakazi mwenzake parokiani.

Taarifa ya Polisi imedai kuwa wawili hao waliingia hotelini siku ya Ijumaa (Julai 7 usiku) kwa mapumnzoko, na ilipofika Julai 8 saa 8 usiku mwanamke wake alitoa taarifa kwa wahudumu wa hoteli hiyo kuwa Wanjiku alikuwa akipata kizunguzungu na kupoteza fahamu, ambapo alifariki dunia kabla ya kufikishwa Hospitalini.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mwili wa Padri huyo ulikutwa umefunikwa nusu na shuka la kitanda cha hoteli hiyo, huku povu jeupe likitoka puani na mdomoni.




Post a Comment

0 Comments