ATHUMANI Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amewashangaza watu wengi kwa kuamua kufunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai kuwa lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo,Athuuman amesema aliamua kuoa wanawake wanne baada ya kupata hasira kwa aliekuwa mke wake kumuacha, ndio ikapelekea kuoa wanawake wengi ili ikitokea tena mke mwingine kumuacha basi atabaki na hao wengine, ameongeza kuwa haikuwa kazi rahisi lakin alifanikiwa kuwapata na ilichukua mda mrefu kuwashawishi mpaka wakamkubalia kwa pamoja.
0 Comments