Ticker

7/recent/ticker-posts

MAYELE HAONDOKI YANGA, UONGOZI WAMALIZANA NAE KIMYA KIMYA

Mshambuliaji kinara wa timu ya Yanga, Fiston Kalala Maayele, ataendelea kusalia kwenye kikosi cha timu ya Yanga hadi mwaka 2026.

Awali kuliibuka tetesi za kupndoka kwa mshambuliaji huyo hatari  raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo (DRC).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu ya Yanga, sasa makubaliana yamekamilika na tayari mchezaji huyo ameongeza miaka miwili zaidi kutoka kwenye Mkataba wake wa mwaka mmoja.

Mkataba mpya wa Mayele na Yanga umeboreshwa kwa kiasi kikubwa, ambapo Sasa atapokea mshahara wa shilingi milioni 40.Makubaliano hayo yameweka wazi kuwa mshahara wa milioni 40 utahusu miaka miwili aliyoiongeza huku mshahara wa awali wa shilingi milioni 16 ukiendelea kutumika kwenye mwaka mmoja wa mwisho wa mkataba wake wa zamani.

Post a Comment

0 Comments